Baadhi
ya Waandishi wa habari wakifanya kazi yao na kuelekezwa namna (Cath
Lab) mtambo wa kufanya uchunguzi na kuzibua mishipa ya damu inayopeleka
damu kwenye moyo na pia kuziba matundu ndani ya moyo bila kufungua
kifua.
Katikati ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili
Dkt. Hussein Kidanto akizungumza na waandishi wa habari. Kushoto ni
Prof. Jameel Alata ambaye ni Daktari Mwelekezi wa Magonjwa ya Watoto
ambaye ameongoza timu ya madaktari bingwa kutoka Hospitali ya Prince
Sultan Cardiac Centre iliyoko Riyadhi nchini Saudi…
Baadhi
ya Waandishi wa habari wakifanya kazi yao na kuelekezwa namna (Cath
Lab) mtambo wa kufanya uchunguzi na kuzibua mishipa ya damu inayopeleka
damu kwenye moyo na pia kuziba matundu ndani ya moyo bila kufungua
kifua.
Katikati
ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili Dkt.
Hussein Kidanto akizungumza na waandishi wa habari. Kushoto ni Prof.
Jameel Alata ambaye ni Daktari Mwelekezi wa Magonjwa ya Watoto ambaye
ameongoza timu ya madaktari bingwa kutoka Hospitali ya Prince Sultan
Cardiac Centre iliyoko Riyadhi nchini Saudi Arabia ambao watakuwepo
Muhimbili kwa siku tisa kuanzia tarehe 8 hadi 16 Mei, mwaka huu. Kulia
ni Sheikh Said Ahmed Abri ambaye ni Mwenyekiti Mtendaji wa Shirika
lisilo la Kiserikali la Kiislam la hapa nchini liitwayo Dhi Nureyn
Islamic Foundation na shirika hili ndilo lililoratibu timu hii ya
madaktari kuja kutoa huduma.
Baadhi ya madaktari bingwa kutoka Hospitali ya Prince Sultan Cardiac Centre iliyoko Riyadhi nchini Saudi Arabia wakimsikiliza Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili wakati akiwakaribisha na kuzungumza na vyombo vya habari, leo Jijini Dar Es Salaam.
Mwezi Mei tarehe 9, mwaka 2015, Tanzania imeandika historia nyingine
baada ya kufanya Tiba ya moyo bila ya kufanya upasuaji kwa kuziba
matundu yaliyoko kwenye moyo kwa kutumia “kifaa maalum” bila kufungua
kifua kama ilivyozoeleka.Baadhi ya madaktari bingwa kutoka Hospitali ya Prince Sultan Cardiac Centre iliyoko Riyadhi nchini Saudi Arabia wakimsikiliza Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili wakati akiwakaribisha na kuzungumza na vyombo vya habari, leo Jijini Dar Es Salaam.
Tiba hii inafanyika kwa mara ya kwanza nchini kupitia Idara ya Tiba na Upasuaji Moyo ya Hospitali ya Taifa Muhimbili ikishirikiana na madaktari bingwa kutoka Hospitali ya Prince Sultan Cardiac Centre iliyoko Riyadhi nchini Saudi Arabia ambao watakuwepo Muhimbili kwa siku tisa kuanzia tarehe 9 hadi 16 Mei, mwaka huu.
Madaktari hawa wamekuja kupitia taasisi ya Al Mutanda Islami Trust ya Uingereza. Akizungumza na wanahabari, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili Dkt. Hussein Kidanto amesema jumla ya wagonjwa zaidi ya 20 wanatarajiwa kupatiwa tiba hii.