Header ads

Header ads
» » Ngassa amfunika Samata kwa mkwanja,Wasauz wamlipa Sh Mil 300

MSHAMBULIAJI mpya mwenye kasi wa Free State Stars ya Afrika Kusini, Mrisho Khalfan Ngassa (26) ameweka rekodi mpya ya usajili nchini kwa wazawa.

Rekodi ya usajili kwa wazawa na wageni inashikiliwa na Emmanuel Okwi ambaye aliuzwa na Simba kwenda Etoile du Sahel kwa dola 300,000 (Sh milioni 480 wakati ule), hata hivyo malipo hayo hadi leo ni ‘hadithi’ tu.
Ngassa anakuwa Mtanzania aliyenunuliwa bei ghali zaidi nje ya Tanzania akimpiku mshambuliaji wa TP Mazembe, Mbwana Samatta.




Ngassa amenunuliwa na Free State Stars kwa kitita cha Rand milioni 1.7, sawa na dola 150,000 (zaidi ya Sh milioni 300).
Wakati Samatta aliyejiunga na Mazembe msimu wa 2011-12 akitokea Simba alinunuliwa kwa kitita cha dola 100,000 (zaidi ya Sh milioni 200), Ngassa amejiunga na Free Stats Stars iliyo katika mji mdogo wa Bethlehem kwa kitita hicho akiwa mchezaji huru.

Ingawa uongozi wa Free State Stars na Ngassa mwenyewe wamekuwa wakifanya siri kubwa, lakini jarida namba moja la soka nchini Afrika Kusini la Kickoff, limethibitisha kuwa Ngassa amelipwa kiasi hicho cha fedha kwa mkataba wa miaka minne.

Kwa kitita hicho alichopewa Ngassa cha Rand milioni 1.7, sasa ndiye mchezaji ghali zaidi katika kikosi hicho kinachonolewa na Kocha Mmalawi, Kinnah Phiri.Wakati anaondoka, Ngassa alikuwa mchezaji ghali zaidi kutokana na uhamisho wake Yanga kwenda Azam. Aliuzwa kwa dola 45,000. Kutoka Azam kwenda Simba ilikuwa mkopo lakini akalipwa Sh milioni 25 na gari. Kutoka Simba kwenda Yanga, alikutana na tatizo na kulazimika yeye kudaiwa Sh milioni 45 na Simba.

Ngassa amejiunga na timu hiyo akiwa mchezaji huru, hivyo kumfanya afaidike zaidi na fungu hilo pamoja na wakala wake.
Mchezaji mwingine ambaye alinunuliwa kwa fedha nyingi ni Mwinyi Kazimoto ambaye Al Markhiya ya Qatar ilimwaga dola 50,000 (zaidi ya Sh milioni 100) kwa Simba ili imnase.

Mchezaji mwingine aliyenunuliwa kwa kitita kama hicho ni Haruna Moshi ‘Boban’ ambaye Simba ililamba dola 50,000 kutoka kwa Gefle IF ya nchini Sweden.TP Mazembe ilitoa kitita cha dola 40,000 kumpata Thomas Ulimwengu ambaye alikuwa amejiunga na kituo cha AFC Academy cha jijini Stockholm nchini Sweden.

Imehaririwa na;- Unknown

Habari yako! Endelea kutembelea Tovuti ya TeknoTaarifa kwa Taarifa murwa za Teknolojia kutoka ndani na nje ya Tanzania, Tupo kwa ajili ya wapenzi wa Teknolojia.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post