Kwa mujibu wa wakazi walioshuhudia fedha hizo wameiambia hivisasa Blog kwamba fedha hizo zipo katika mafungu ya shilingi elfu moja, elfu tano pamoja na elfu kumi.
Inadaiwa kuwa fedha hizo zilianza kuonekana kuanzia jumanne ambapo leo ndio imebainika kwamba zipo kwa wingi katika Bonde hilo.
Kufutia tukio baadhi ya mama ntilie ,Wachoma chipsi wamemiminika katika bonde hilo kuzichukua fedha hizo kwa lengo la kupikia, huku watoto wakizichezea.
Naye mjumbe ambaye haukutaka kutaka jina lake amesema kwamba fedha hizo zinadaiwa kutoka Benki Kuu kwenda kutupwa Bonde la Pugu lakini cha kushangaza zimetupwa katika bonde hilo.
Mamia wa wananchi wamemiminika kwenda katika bonde hilo kujionea fedha hizo ambapo asilimia kubwa ya wananchi wamesema hawajawahi kuziona fedha nyingi kiasi hicho.
Mtandao wa hivisasa unaendelea kuwatafuta viongozi katika eneo hilo na tutakujulisha kinachoendelea.