Header ads

Header ads
» » MTOTO MKUBWA ZAIDI AZALIWA NCHINI MAREKANI

Avery mtoto mkubwa kuliko kawaida nchini Marekani
Mwanamke mmoja nchini Marekani amejifungua mtoto mwenye uzito wa paundi 14.1 sawa na kilo 6.4kg na sasa mtoto huyo anakula mara mbili zaidi ya uwezo wa mtoto mchanga .
BiMaxxzandra Ford amepata mtoto aliyempa jina Avery, ndiye mtoto mkubwa na mzito kuwahi kuzaliwa katika hospitali ya wanawake ya mtakatifu Joseph iliyoko Tampa, Florida.Avery, alizaliwa kwa njia ya kawaida .
Ford alikuwa hajatanabahi kuwa yu mjamzito mpaka alipotimiza wiki 35 .lakini mara baada ya kuwa anaongezeka uzito kupita kiasi ,madaktari wakamthibitishia kuwa yu mja mzito,na kutokana na kasi ya unenepaji mwanzo Bi Ford alihisi atajifungua watoto pacha,kumbe sivyo.
Debbie Moore, mkunga katika hospitali hiyo, wasingemruhusu mwanamke huyo ajifungue kwa njia ya kawaida kama wangegundua mapema ana mtoto mwenye kilo nyingi kiasi hicho .
Avery anabaki hospitalini chini ya uangalizi maalumu tangu alipozaliwa tarehe 29 January , lakini anatarajiwa kuruhusiwa kwenda nyumbani hivi karibuni .
Bi Ford, anaye mtoto mmoja mwenye umri wa mwaka mmoja na mtoto wa kike mwenye miaka mitano.

SOURCE:: BBC HABARI

Imehaririwa na;- poatel Africa

Habari yako! Endelea kutembelea Tovuti ya TeknoTaarifa kwa Taarifa murwa za Teknolojia kutoka ndani na nje ya Tanzania, Tupo kwa ajili ya wapenzi wa Teknolojia.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post