Header ads

Header ads
» » UCHAGUZI WANUKIA:RIDHIWAN AJIPANGA KIKAMILIFU HUKO CHALINZE

Mbunge wa Jimbo la Chalinze, Ridhiwani Kikwete (kulia), akipata maelezo kutoka kwa Msimamizi wa ujenzi kutoka Kambi ya Mzinga ya JWTZ, Aloyce Mayunga (kushoto) alipokwenda kukagua ujenzi wa maabara ya Shule ya Sekondari ya Kiwangwa wakati wa ziara ya kikazi ya katika Kata ya Kiwangwa, wilayani Chalinze, Pwani leo.Aliwataka wajenzi hao kujenga maabara hayo kwa kuzingatia viwango. Katikati ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Wilaya ya Bagamoyo, Saleh Mpimbwi.

 Ridhiwani Kikwete akizungumza na wakandarasi kutoka Kambi ya Mzinga ya JWTZ wanaojenga maabara ya Shule ya Sekondari ya Kiwangwa wakati wa ziara ya kuagua miradi ya maendeleo na kuwashukuru wananchi kwa kumchagua kuwa mbunge miezi sita iliyopita.

 Ridhiwani akinyoosha juu kadi ya Chadema aliyokabidhiwa na aliyekuwa Mwenyekiti wa  Chadema Kijiji cha Masugulu ambaye amehamia CCM katika mkutano wa hadhara katika Kijiji cha Mwitemo Kata ya Kiwangwa leo

 Ridhiwani akihutubia wananchi  katika Kijiji cha Mwitemo

 Sehemu ya akina mama wakisikiliza kwa makini wakati Ridhiwani Kikwete akihutubia katika Kitongoji cha Magogoni, Kijiji cha Msinune, Kata ya Kiwangwa.

 Ridhiwani Kikwete akihutubia wananchi katika Kijiji cha Msinune, Kata ya Kiwangwa.

 Msanii kiongozi wa Kikundi cha sanaa cha Chanzala akifanya maajabu yake wakati mkutano wa hadhara uliohutubiwa na Ridhiwani Kikwete katika Kata ya Kiwangwa



 Mwenyekiti mpya wa Serikali ya Kijiji cha Kiwangwa, Kata ya Kiwangwa, akifungua rasmi mkutano wa hadhara uliohutubiwa na Mbunge wa Jimbo la Chalinze, Ridhiwani Kikwete katika Kata ya Kiwangwa ambapo pamoja na kusikiliza kero zao aliwashukuru wananchi kwa kumchagua mwaka jana.



 Mkazi wa Kiwangwa Shabani Dume akiuliza swali kwa kumtaka Mbunge Ridhiwani asaidie kuwepo dampo katika Kijiji cha Kiwangwa

Imehaririwa na;- poatel Africa

Habari yako! Endelea kutembelea Tovuti ya TeknoTaarifa kwa Taarifa murwa za Teknolojia kutoka ndani na nje ya Tanzania, Tupo kwa ajili ya wapenzi wa Teknolojia.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post