Mwanamke (Zuhura Sudi) anayetuhumiwa kuwaua watoto wake.
Tukio
hilo ambalo limeishangaza nchi hasa kufanywa na mama mzazi ambaye
anaujua uchungu wa kuzaa, lilijiri Jumapili usiku ndani ndani ya nyumba
ya mwanamke huyo.
SIKU MOJA KABLA
Taarifa
kutoka vyanzo vya uhakika, siku moja kabla ya tukio, mwanamke huyo
ambaye ni mtata kiasili alionekana akicheza na watoto wake na watoto wa
jirani huku akionesha uchangamfu mkubwa.
“Kama wale watoto wake wangejua mama yao mzazi ndiyo safari ya kifo chao naamini wasingemchangamkia mama yao.
“Walicheza
kwa amani, kwa upendo. Kumbe mama ana mahesabu yake. Haiwezekani leo
niambiwe kuwa mawazo ya kuwaua watoto wake aliyapata ghafla,” alisema
shuhuda mmoja.
Mtuhumiwa akiwa chini ya ulinzi.
USIKU, JIRANI ASIKIA KISHINDO
Jirani mmoja na nyumba ilipotokea tukio alisema:
“Mimi awali ya siku ya kuelekea usiku wa tukio, nilimwona yule mama. Nikasalimiana naye. Alionekana yupo kawaida tu.
“Lakini
usiku, kukiwa kumetulia nilisikia vishindo kama mtu anachimba ardhi.
Nilipofuatilia nikabaini vilikuwa vikitoka upande wa nyumbani kwa
mwanamke yule.“Sikushtuka. Nilijua ni shughuli zake za kawaida
zinaendelea ndani ya nyumba yake. Kulipokucha sasa, nikasikia yule mama
anasema kwamba watoto wake wamepotea.
“Palepale
nikaanza kuhisi kitu kwa ile mishindo ya usiku. Inaonekana alishawaua
watoto wake sasa alikuwa anachimba mashimo ya kuwafukia. Kule si
kuwazika na yale si makaburi ni mashimo.
“Inauma sana, siamini kama mama aliyezaa watoto kwa uchungu mkubwa anaweza kufanya ukatili kama huu.”
Miili ya watoto hao baada ya kufukuliwa kwenye mashimo.
AKILI ILIMWAMBIA ASUBIRI AKIWA PEKE YAKE
Baadhi
ya majirani walisema ndani ya nyumba hiyo kuna watu wengine wanaishi,
lakini mtuhumiwa huyo alisubiri akiwa peke yake ndipo akatekeleza
ukatili wake wa kutisha.
ANACHOJUA MWENYEKITI WA MTAA
Kwa
mujibu wa Mwenyekiti wa Mtaa wa Utusi, Aziza Mwenya, ushirikiano
mkubwa kati ya wananchi wa mtaa huo ndiyo uliofanikisha
kugundulika kwa tukio hilo la kinyama lililopoteza maisha ya
watoto hao wasiokuwa na hatia.
“Baada
ya kupokea taarifa kutoka kwa babu wa Zuhura, mzee Shaban
Ramadhan kuhusu kutoweka kwa watoto hao katika mazingira ya
kutatanisha, tulifika kwenye nyumba ya tukio kwanza na kumhoji mama wa
watoto.
Ndugu na majirani wakiwa na makamanda wa Polisi eneo la tukio.
“Cha
ajabu alikuwa akizuia watu kuingia ndani. Kumbe alishajua
kinachoendelea na akiruhusu sisi kuingia nini kitatokea.“Hata hivyo
majirani kwa kushirikiana na mimi na baba wa mmoja wa watoto waliouawa
(Sudi Mrisho), Mrisho Abdallah tulimshika kwa nguvu Zuhura, watu
wakaingia.”
WAKUTA MASHIMO MAWILI
“Tulipofika,
tukabaini mashimo mawili aliyokuwa amewafukia watoto wake. Shimo moja
sebuleni, jingine chumbani. Tuliwapa taarifa polisi wakafika haraka
sana. Mashimo yalipofukuliwa, watoto walikutwa ndani ya mifuko miwli ya
sandarusi. Inauma sana. ”
MTUHUMIWA AZUNGUMZA
Amani
lilibahatika kuzungumza na mwanamke huyo katika mahojiano mafupi akiwa
chumbani muda mfupi kabla ya polisi kufika.Amani: “Hivi Zuhura, ni
kwanini umeamua kuwaua watoto wako wa kuwazaa?”
Zuhura: “Nani? Mimi sijui, we (mwandishi) ndiyo unajua.”Amani: “Watoto wako wako wapi?”
Zuhura: “Nani? Wako wapi kwani?”
KILICHOONEKANA
Baadhi
ya wakazi wa eneo hilo walisema, Zuhura licha ya kuonekana hana
wasiwasi wowote, lakini pia aliashiria kujitoa ufahamu ili atafsirike
kwamba hakuwa na akili timamu.
KUMBUKUMBU MBAYA
Kwa
mujibu wa taarifa kutoka kwa majirani zinadai kuwa, mwaka 2013, Zuhura
alidaiwa kumsababishia kifo mtoto wake mchanga wa kiume kufuatia
kumzidishia dozi ya malaria wakati alipokuwa akiumwa.
KAMANDA WA POLISI
Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora, ACP Juma Bwire ilikiri kutokea kwa tukio hilo.
Afande Bwire alisema mtuhumiwa atafikishwa mahakamani baada ya upelelezi kukamilika.