Yasemekana kuwa Zanzibar ndio ilikuwa ya kwanza barani Afrika kutumia Televisheni (Luninga) zenye rangi mwaka 1973.Na Tanzania Bara walianza kutumia Televisheni (Luninga) zenye rangi miaka 20 baadaye mwaka 1994.
Katika
sherehe za kutimiza miaka kumi ya Mapinduzi 1974, Mwalimu Nyerere
alikuwapo Zanzibar kufungua rasmi Televisheni Zanzibar TVZ ambapo kwa
wakati huo ilikuwa ndiyo TV ya kwanza ya rangi Afrika.
Pichani
Ni Mkurugenzi wa TVZ Antony Mendis kulia kwa Mwalimu, Kamishna wa
Polisi Zanzibar Edington Kissasi (Marehemu), Rais wa Zanzibar Aboud
Jumbe Mwinyi nyuma ya Mwalimu, Waziri Kiongozi Ramadhaan Haji Faki
aliyevaa baraghashia na Shaaban Mloo (Marehemu) nyuma ya Mendis.