Jopo la wataalamu waliokutana huko Geneva katika mkutano uliandaliwa na shirika la Umoja wa Mataifa la UNCTAD, limesisitiza haja ya kuwa sera zinazoangazia maeneokamasayansi, teknolojia na ubunifu kwa kusema kuwa ni muhimu kwa ajili ya kusuma mbele maendeleo.Aidha wataalamu hao walisema kuwa suala la utungwaji wa sera na kuzitekeleza inasalia kuwa changamoto kubwa inayowakabili watunga sera.
Mkutano huo uliwaleta pamoja magwiji wa sera katika eneo la sayansi, teknolojia na ubunifu ambako walijadilia mbinu zinazoweza kutumika ili kusuma mbele kile kinachoitwa ufanisi katika uandaaji na utelezwaji wa sera.
Katika majadiloanoyaowataalamu hao walibainisha haja ya kuwa na utashi wa kisiasa ili kufanikisha mipango ya muda mrefu ya uletaji maendeleo. Kulitolewa pia uzoefu uliojitokeza katika baadhi ya mataifa ambayo yameonyesha mfano wa kuigwa kuandaa na kutekeleza sera zinazochochea maendeleo ya sayansi na teknolojia.
Kwa hivi sasa UNCTAD imekuwa ikiendesha mradi wa majaribio katika mataifa kadhaa, na taarifa za awali zinaonyesha kufanya vizuri mradi huo unaohusu sera na maendeleo.Ghanani moja ya nchi ambazo mradi huo unatajwa kufanya vizuri.
Source: unmultimedia.org