Serikali ya Rwanda kuanza kutumia ndge zisizokuwa na rubani kusafirisha dawa zinazohitajika kila mara katika mikoa ambayo iko mbali.
Maisha ya wagonjwa wengi ambao huhitaji matibabu ya dharura huwekwa katika hali ya hatari kwani dawa huchelewa kufikia mahali ambapo zinahitajika .
Aidha ndege hizo pia zitatumika katika kusafirisha damu zinazohitajika katika vituo 21 vya afya nchini humo.
Mnamo mwezi Februari Rwanda na kampuni moja ya California ya kutengeneza roboti na ndege zisizo na rubani zilitia saini ya kuleta ndege hizo ili kuhamasisha usafirishaji wa vifaa vya matibabu kwa haraka .
Wizara ya Afya nchini humo tayari ilithibitisha kueletwa kwa ndege 15 kwa ujumla .
Chanzo: dailydot.com