Header ads

Header ads
» » Kampuni ya Huawei imeshika namba moja katika Mauzo

Huawei imeyatupa mbali makampuni mengine kama vile Apple ambao wameshika namba tano na wapinzani wao wengine, Samsung ambao hawajashika hata tano bora. 
The lineup of various Huawei P9 colours
Taarifa hizi zimetolewa na mtandao wa IDC. Katika repoti ambayo mtandao huo ulitoa ni kwamba huawei ilisafirisha simu milioni 19.1 mpaka mwezi wa 6 mwaka 2016. Na hiyo ni 15.2 % ya ongezeko la namba ya simu zilizouzwa na kampuni hiyo katika kipindi cha nyuma. Kwa sasa kampuni ya Huawei ndio imeshikilia namba moja huku ikifuatiwa na OPPO na Vivo (wote hawa wanajihushisha na simu za kijanja pia). Kwa upande wa Xiaomi soko limeshuka kwani waliuza simu milioni 10.5 wakati msimu uliopita ndio walishikilia usukani kama vinara (namba moja) kwa kuuza simu milioni 17.1 katika msimu uliopita. Apple na wenyewe ni majanga (lakini inafahamika kuwa nchini China huwa wafanyi vizuri licha ya simu zao kuwa bei ghali) wameuza simu milioni 8.6 na hiyo namba imeshuka kwani awali waliuza simu nyingi zaidi ya hizo. 
 
Hii ndiyo Ripoti ya IDC 
Hata hivyo kampuni ya Xiaomi imepingana na ripoti hiyo na kuomba kuwa kampuni lingine liweze kusimamia upya ripoti hiyo kwani ina makosa. Wao Xiaomi wanasema kuwa waliuza simu milioni14.2, japokuwa katika repoti ya IDC bado hata ukichukua hiyo namba bado Xiaomi wanakuwa katika nafasi ya nne. Lakini bado Xiaomi hawaamini kwani kama wameweza kukosea kwao, wanaweza wakakosea na kwingine – Xiaomi wakisema hivyo. Apple kwa upande mwingine mauzo yake yanazidi kushuka sana katika soko la china, kumbuka hata simu yake ya iPhone 5se haikufanya vizuri sana kwani watu wengi walihitaji simu zenye vioo vikubwa. 
xiaomi phone 
Simu za Xiaomi
Cha muhimu kuzingatia hapa ni kwamba taarifa hizi ni mauzo ya robo ya pili ya mwaka 2016 kwa mauzo ya soko la simu huko nchini china 

Chanzo: idc.com/

Imehaririwa na;- poatel Africa

Habari yako! Endelea kutembelea Tovuti ya TeknoTaarifa kwa Taarifa murwa za Teknolojia kutoka ndani na nje ya Tanzania, Tupo kwa ajili ya wapenzi wa Teknolojia.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post