Sasa barani Afrika kuna zaidi ya
watumiaji wa simu milioni 700 na zaidi, hii ni mara nane zaidi ya idadi ya watumiaji wa
simu za mkononi Afrika toka mwaka 2000,
kulingana na ripoti iliyotolewa na Chama cha Mawasiliano ya Kimataifa
(International Telecommunication Union--ITU).
Ripoti hiyo ilionyesha kuwa
teknolojia ya simu imekuwa muhimu katika kukuza ushirikino wa kibiashara barani Afrika; na pia kuwezesha mawasiliano
ya simu za kimataifa kuongoza kupanua bidhaa zao na kushindana kwa sehemu ya
soko.
Simu za mkononi sasa utoa huduma za
kibenki katika nchi nyingi Afrika, nchi zinazoongoza kwa huduma hizo ni Kenya, Uganda, Tanzania,Ivory
Coast, Zimbabwe, Botswana, Rwanda na Afrika Kusini.
CHANZO: International Telecommunication Union (ITU)
MHARIRI: AbdallahMagana.com