Leo nakufundisha jinsi ya kuweka mipangilio (setting) flani
kuiwezesha kompyuta kujizima pale muda flani utakapofika au ata pale tuu
ambapo itakuwa haitumiki.
Kufanikisha jambo hili itabidi uifahamu programu iitwayo ‘Task Scheduler’!
Unaweza ipata kwa kubofya ‘Start’ kisha tafuta kwa kuandika ‘Task Scheduler’
au kwa Windows 7 bofya ‘Start’ → ‘Control Panel’ → ‘System and
Security’ → ‘Administrative Tools’ → ‘Task Scheduler’. Na kama unatumia
toleo la Windows 8, basi bofya ⊞ Win key, kisha andika “schedule tasks”, na bofya kuchagua “Schedule tasks” katika matokeo.
Bofya ‘Create Basic Task’,
kisha andika taarifa zozote muhimu za kukufanya ukumbuke pale
utakapoondoa au kutaka kufanya mabadiliko siku flani. Asaasa jaza sehemu
ya jina – ‘name’, kwenye maelezo sio muhimu. Kisha ‘BOFYA NEXT’
Unaweza chagua kama ni kila siku, au mara moja kwa wiki n.k
Kwa kuwa tunataka iwe kila siku basi chagua ‘Daily’ kisha bofya ‘NEXT’. Hapa utaona sehemu za kuweka muda unaotaka kompyuta iwe inajizima, sehemu ya ‘Recur every X Days’ yenye maana ya hali hiyo ijirudie kila baada ya siku X, acha iwe 1 (Moja), kisha ‘BOFYA NEXT’
Kisha bofya ‘NEXT’
Kiuhalisia kompyuta inapozimika kuna programu ya ndani kabisa inayofanya kazi hiyo, basi kwenye eneo la “Program/script” andika, C:WindowsSystem32shutdown.exe au unaweza kukopi na ku’paste’ moja kwa moja kama tuliivyoandika hivyo
Eneo la “Arguments” andika /s
Bofya ‘NEXT’
…..vile unavyotaka kiwe, unaweza badilisha jina tena la kumbukumbu.
Kama umeridhika na kila kitu basi bofya ‘Finish’
Tayari! Sasa tegemea kila siku katika muda ule uliouchagua kompyuta yako itakuwa inajizima yenyewe.
Kumbuka kama utataka kufanya mabadiliko au kuanza upya kabisa na kuondoa chaguo basi fungua tena programu ya Task Scheduler kisha bofya ‘Task Scheduler Library’,
moja ya chaguo litakalokuwa linaonekana upande wa kushoto. Ukibofya
utaona jina kama ulivyolichagua katika vitu vilioorodheshwa, basi
utaweza kufuta au kubofya na kufanya mabadiliko.
CHANZO: wikihow.com
MHARIRI: Abdallah Magana
Topics: ELIMU
Imehaririwa na;- poatel Africa

Habari yako! Endelea kutembelea Tovuti ya TeknoTaarifa kwa Taarifa murwa za Teknolojia kutoka ndani na nje ya Tanzania, Tupo kwa ajili ya wapenzi wa Teknolojia.
Soma na Hizi
hatua 5 muhimu za kupitia kama unaitaji kumiliki website
Kama wewe ni mfanyabiashara wa kati au juu, basi kuwa na Website ni moja ya vitu vya lazima kwa...Read more »
22Jan2017Fahamu Jinsi ya Kukabiliana na Mwanga wa Vifaa vya Kieletroniki
TAKRIBAN watu milioni 30 nchini Tanzania wanatumia simu za viganjani na haiwezi kupita siku bil...Read more »
26Aug2016Jinsi ya kutumia intanet kwa simu ya blackberry bila kutumia blackberry internet service
Kwa watumiaji wa Blackberry mtakuwa mnafahamu vyema kwamba simu za Blackberry zinavifurushi v...Read more »
25Aug2016Fahamu Jinsi ya kutumia sim card zote kwenye modem bila ku-Unlock
Habari yako msomaji wa TeknoTaarifa tuendelee kuhabarishana na kujuzana kuhusu haya maujanja...Read more »
24Aug2016Zifahamu faida za Kusoma kwa njia ya mtandao
Kukua na Kuongezeka kwa teknolojia , Kumerahisisha mambo na kuongezeka kwa idadi kubwa ya watu we...Read more »
22Aug2016Njia mbadala za kuhifadhi Taarifa (Faili) zako Mtandaoni
Uzuri wa Teknolojia ni kwamba kama uko makini basi hutaweza kupoteza taarifa zako zozote ambazo ...Read more »
05Aug2016

Playstore
TeknoTaarifa Video
TAARIFA ZILIZOSOMWA SANA
-
Computer ina uwezo wa kufanya mambo ambayo binadamu...
-
Mambo vipi Rafiki yangu? Kama wewe ni miongoni mwa...
-
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala...
-
BEST TANZANIAN UNIVERSITIES 2015: Latest Rankings ...
-
Coca-Cola Kwanza Limited of Dar es Salaam, is part...
-
Kampuni ya Samsung Electronics Co Ltd imeanza...
-
Kwa wale Rafiki zangu wa ma-gadgets and all...
-
Si wengi wetu wanaofahamu umuhimu wa kula samaki mara...
Data Boosta
