Kituo ambacho ni kikubwa zaidi kwa Afrika Mashariki. Hii ni katika harakati za serikali kuhakikisha kwamba haibaki nyuma katika mbio za Tehama kwa nchi za Afrika mashariki.
Data
centre hiyo ambayo ina miundombinu ya kisasa na madhubuti itakuwa
inahost huduma za database kwa taasisi za serikali na pia taasisi za
sekta binafsi. Hili litasaidia kushusha gharama za kufanya
hudma hizo maana kwa sasa watu wengi wamekuwa waki zifuata huduma hizi
huko ng’ambo.
Benki ya Exim ya China ilitoa msaada wa dola za kimarekani milioni 93.7 kwa ajiri ya kujengwa data centre tatu pamoja na kuendeleza mradi wa mkonga wa taifa wa fibre. Vituo vingine vitafungwa huko Zanzibar na Dodoma katika awamu zinazokuja.
Kituo cha data hiki kipo katika hatua za mwisho mwisho katika kuanza kazi na inategemewa pengine kitaanza kazi mwezi wa nne.
TTCL kwa niaba ya serikali ndio watakao
kuwa wanasimamia mawasiliano katika kituo hiki, wakati Huawei wao ndio
watakao hudumu kama washauri wakuu wa serikali juu ya masuala ya
kiteknolojia katika kituo hiki.
Mpaka sasa kuna zaidi ya vijana mia moja
wamepelekwa kwenda kusoma China ili kuwezesha serikali kuwa na nguvu
kazi ya kutosha, na zaidi ya hayo wamekwisha kuja wataalamu mbalimbali
kwa ajiri ya kuwafundisha wazawa.
Kituo hiki pia sio tuu kikubwa kwa
Afrika Mashariki bali pia kinaendeshwa na umeme wa nguvu za jua, hii
inafanya gharama za uendeshaji wa kituo hiki pindi kitakapoanza zisiwe
kubwa sana.
CHANZO: africanbusinessnetwork
MHARIRI: AbdallahMagana Website