Canonical, shirika linalomiliki
programu endeshaji maarufu ya Ubuntu iliyo katika familia ya Linux ndio walifanikiwa
kuingiza sokoni simu ya kwanza inayotumia programu endeshaji (OS) ya Ubuntu. Na
mafanikio yamekuwa makubwa sana kwani simu hiyo ilifanikiwa kuuza nakala zote
walizokuwa nazo ndani ya muda mchache. Programu endeshaji ya Ubuntu inategemea
kuingia ushindani na za iOS na Android, je watafanikiwa? ni mapema sana kusema.
Simu hiyo kutoka kampuni ya Ulaya ya
BQ inayofahamika kwa jina la BQ Aquaris E4.5 Ubuntu Edition ilizinduliwa February,
2015 na iliuzika kwenye mtandao wa
watengenezaji wa simu hiyo. Ubuntu wamejitahidi kwenye ubunifu wa kitofauti na
mvuto, wanategemea kujifunza mengi kutoka mafanikio ya Android ambayo nayo
imejengwa juu ya mfumo wa Linux.
Simu ya BQ Aquaris E4.5 Ubuntu
Edition inapatikana kwenye soko la Ulaya kwa takribani dola za kimarekani 190.
Sifa
za Simu hiyo;
Kioo cha inchi 4.5 (960×540) a
quad-core 1.3GHz Cortex A7 CPU RAM GB 1 Diski uhifadhi GB 8 (Unaweza tumia kadi
ya SD hadi ukubwa wa GB 32 Kamera ya nyuma ‘megapixel’ 8 na ya mbele megapixel
5
Mafanikio ya toleo hilo yatasaidia
kuonesha uhitaji (demand) na umaarufu wa programu endeshaji hii, yapo makampuni
mengine ya simu yanayotegemewa kuleta simu zinazotumia Ubuntu kipindi cha mwaka
huu na mwakani. Wengi wanataka Ubuntu ipate mafanikio katika soko linaloonekana
kumilikiwa na Android na iOS kwa sasa, wengi wanasema ni muhimu kuwe na
ushindani mkubwa wa kampuni tatu kuliko mbili. Windows na BlackBerry OS
hawajafanikiwa sana kuonesha ushindani wa uhakika na ujio wa Ubuntu
unakaribishwa vizuri lakini ni ukweli usiopingika wana kazi kubwa ya kufanya
kuhakikisha mafanikio ya programu endeshaji hii. Kampuni ya Canonical walifanikiwa
kuleta simu inayotumia ubuntu.
CHANZO: techrepublic.com
MHARIRI: Abdallahmagana.com