kampuni ya HP ilitengeza kompyuta ya kitofauti zaidi kuliko zote ambazo zimeshawahi kuingia sokoni. Nayo ni HP Sprout! Hii ni kompyuta ambayo imeenda kinyume na muonekano wa kompyuta wa zaidi ya miaka 35 ya utengenezaji wa kompyuta.
Sifa za Kompyuta hiyo
Kwanza kabisa imefuta utumiaji wa kibodi (keyboard) kama tulivyozizoea. HP Sprout inakupa kajikamkeka (mat) cha kioo ambacho kina sensa za mguso (touch) hivyo kazi za kibodi na mausi zinachukuliwa na eneo hili.Kitu chochote utakachoandika au kuchora katika eneo hili kitakuwa pokelewa na kompyuta. Pia kupitia kamera ya 3D iliyopo kwenye eneo la juu, kompyuta itaweza kupokea picha ya kitu chochote utakachoweka katika kajimkeka hako, yaani itapiga picha ya kitu/umbo husika, na utaweza kufanyia maboresha ya kiubunifu kwenye programu za ubunifu kwenye kompyuta.
Ukitoa uwezo wa skana (scanner) , kompyuta hii pia inauwezo wa kutumiwa kama projekta . Sifa zote hizi ndani ya kompyuta moja inaifanya HP Sprout kuwa kompyuta ya kitofauti sana. Swali kubwa ni je kompyuta hii ni kwa ajili ya watu gani na kwa matumizi gani?
HP walisema hilo ni swali ambalo wao hawana majibu ya moja kwa moja nalo, wanategemea watumiaji kuweza kugundua wataitumiaje, lakini hadi sasa inaonekana ni kompyuta nzuri zaidi kwa wabunifu, watoto wanaopenda masuala ya sanaa kama uchoraji n.k. Lakini pia ilikuweza kuuza ata kwa watu wanaoitaji kibodi za kawaida ukinunua HP Sprout utapata kibodi na kipanya vya ‘wireless’, yaani visivyotumia waya ili kuweza kukusaidia kutotumia kamkeka ka mguso pale inapobidi. Sifa Kuu Inakuja na Windows 8.1 Kioo inchi 20 Kioo/mkeka mguso inchi 23 Prosesa Core i7 na Gb 8 ya RAM. Kompyuta hii inauzwa kwa dola 1899 za kimarekani, iliingia rasmi sokoni Novemba 9 mwaka 2014
Tazama video hii ya HP Sprout
CHANZO: HP.COM
MHARIRI: Abdallahmagana.com