Teknolojia mpya ya utengenezaji
betri iliyotengenezwa na mwalimu na mwanafunzi wake wa PhD huko nchini Korea
Kusini itawezesha kifaa kama simu kukaa na chaji kwa wiki moja nzima bila
kuchaji. Profesa Choi na mwanafunzi wake wa chuo kikuu cha Pohang wametengeneza
betri la aina ya ‘solid oxide’ {solid oxide fuel cell (SOFC)} wakiwa na lengo
la betri hilo kutumika badala ya betri za sasa hivi ambazo ni za ‘lithium-ion’.
Prof. Choi &
Mwanafunzi wake Kun Joong Kim
Betri zinazotumika katika simu,
tableti, drone na vifaa mbalimbali vya elektroniki kwa sasa ni za teknolojia ya
Lithium-ion. Betri hizi zinakiwango kidogo za uhifadhi wa chaji. Teknolojia hii
iliyogunduliwa na Profesa Choi na mwanafunzi wake, Bwana Kun Joong Kim
imepokelewa vizuri kwani inaweza kutumika ata kwa betri kubwa kama zile
zinazoitajika kwenye magari yanayotumia umeme.
Utengenezaji wa SOFC kutumia TLC
Teknolojia hii inategemea utumiaji
wa Hydrogen, ikiwa pia na sifa ya utengenezaji usio mgumu sana huku
‘electrolyte’ zake zikiwa na sifa kubwa ya kutopotea kwa urahisi – hivyo uwezo
wa kukaa na chaji kwa muda mrefu. Kwa teknolojia hii vifaa kama simu janja
zitaweza kuchajiwa mara moja tuu kwa wiki huku vifaa kama vile drones vitaweza
kutumika kwa zaidi ya lisaa limoja. Hii ni tofauti na sasa ambapo simu nyingi
huchajiwa kila siku huku drone zikiweza kurushwa chini ya lisaa limoja kabla ya
kuitaji kuchajiwa.
Fahamu zaidi Project
CHANZO; postech.ac.kr
MHARIRI; Abdallahmagana.com