Header ads

Header ads
» » kiungo cha mwili chaundwa kwa kutumia kichapishi cha kibiyolojia chenye mfumo wa 3D

 

Wanasayansi wa Urusi wamefanikiwa kutengeza kiungo cha mwili kwa kutumia kichapishi cha kibiyolojia chenye mfumo wa 3D.
Kiungo hicho kiliweza kufanyiwa majaribio ndani ya maabara ya sayansi na kupandikizwa kwa panya kwa mafanikio.
Kulingana na maelezo ya wanasayansi, inaarifiwa kichapishi hicho cha kibiyolojia kitaweza kuunda viungo vya mwili miaka 15 ijayo na kuweza kutumika katika upandikizaji.
Miezi kadhaa iliyopita, kiungo kingine cha mwili kilichoundwa kwa kutumia kichapishi cha kibiyolojia pia kilifanyiwa majaribio nchini Italia.
Wanasayansi wa Italia pia waliwahi kuunda kiungo cha jicho kwa kutumia mfumo huo huo na kutangaza kwamba kitaweza kutumika kwa ajili ya kutatua maradhi ya macho.

Source: Trt News

Imehaririwa na;- poatel Africa

Habari yako! Endelea kutembelea Tovuti ya TeknoTaarifa kwa Taarifa murwa za Teknolojia kutoka ndani na nje ya Tanzania, Tupo kwa ajili ya wapenzi wa Teknolojia.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post