Naamini utakubali kwamba watu wengi tunashukuru mabadiliko ya Sayansi na Teknolojia yamefanya mambo mengi kuwa rahisi sana,
Kwa mfano kipindi cha nyuma sikuku ya valentine ilipokuwa inafika ilibidi kumtumia umpendae au na kadi, mkono kwa mkono, Lakini sasa mambo ni tofauti kabisa, kwani sasa unaweza kutuma Au hata Kadi ukiwa mbali na unayemtumia kwa kutumia mitandao ya kijamii kama Whatsapp, Instagram, Facebook na Twitter.
lakini mabadiliko haya ya Teknolojia yanawapa wakati mgumu wafanyabiashara wa Kadi na Mau.
kwa upande mwingine Matumizi ya mitandao ya kijamii inatajwa kuchangia kuua soko la kadi pamoja na maua yaliyozoeleka kununuliwa msimu huu wa Valentines Day.
Baadhi ya wauza maduka ya kadi na maua
katika maeneo mbalimbali wamelalamikia kuporomoka kwa soko la bidhaa
hizo tofauti na siku za nyuma ambapo zilikuwa zikiuzika kwa kiwango
kikubwa.
Kwa Hali hii inaziilisha wazi kwamba Mitandao ya Jamii imerahisisha mambo mengi zaidi katika jamii, licha ya kuwa kikwazo kwa baadhi ya wafanya biashara. Lakini cha msingi inabidi wabadilike na kwenda na Teknolojia ya sasa, Hapo ubunifu unatakiwa kwa wafanya Biashara.