Mwaka jana, mwana-Kickstarter raia wa Ufaransa aliomba watu wamchangie ili aweze kufanikisha ndoto yake ya kutengeneza kava la simu lenye uwezo wa kusafisha picha na kuzitoa papo hapo, na pia kuipa kava hiyo uwezo wa kutengeneza video ya sekunde tano mara baada ya kupiga picha kupitia kava hiyo.
Kava hiyo ya Prynt sasa imeanza kutumwa kwa wateja walioweka oda mapema baada ya kutambulishwa kwenye mtandao wa Kickstarter April mwaka jana.
Mbali na kuwa na uwezo wa kutoa picha papo hapo, pia kava hiyo ya simu itakua na uwezo wa kugeuza picha hizo kuwa video fupi ya sekunde tano utakazoweza kuziona kupitia simu yako ya mkononi iliyounganishwa na program maalum ya Prynt.
Kwasasa kava hizo zinapatikana kupitia mtandao wake wa www.prynt.co zinazopatikana kwa kiasi cha dola za Kimarekani 149 ambazo ni sawa na takribani Sh. 322,900 za Kitanzania.
Mtandao maarufu duniani wa teknolojia uitwao TechCrunch, ulielezea kava hii katika moja ya makala zake na kufananisha kava hii na mtandao maarufu wa kijamii wa Snapchat.
Prynt pia wametoa ofa maalum ya asilimia 20 kwa msimu huu wa valentine kwa wale wote watakaonunua Prynt kabla ya tarehe 14 February kupitia mtandao wao.
Je hii inaweza kua zawadi nzuri na yakipekee kwa umpendae?
SOURCE; Prynt Website
>>Lengo langu ni kuakikisha upitwi na Habari za Teknolojia ungana Nami FACEBOOK , TWITTER na INSTGRAM