Mafanikio ya teknolojia hii ya chaja
za wireless inakuja kutokana na ukweli kwamba ni rahisi mno kuitumia, ni rahisi
kuweka simu yako juu ya chaja na kuondoka bila ya kushughurika na waya wala
kuchomeka lakini urahisi huu unawezesha teknolojia hii kuwa na matumizi makubwa
zaidi mfano barabarani magari yanayotumia umeme yanaweza kuchajiwa katika mataa
ama katika sehemu za maegesho. Teknolojia hii kimsingi inachukua teknolojia
inayotumiwa na transforma ambapo kwenye chaja yenyewe kuna kuwa na koili ambazo
pindi zinapo pitishiwa umeme hutengeneza nguvu za usumaku ambazo hutumiwa na
koili zilizo katika kifaa chako kutengeneza umeme tena ambao hutumika kuchaji
betri ya simu ama gari ama kifaa chochote husika.
Pamoja na kuwa ni rahisi
kutumia teknolojia hii ya kuchaji vifaa mbalimbali lakini pia teknolojia hii
inatumika zaidi kuchaji vifaa vya baiolojia kama moyo wa bandia kwa kuvichaji
kwake ni njia salama mfano haihusishi kuingiza waya ndani ya mwili, njia hii
pia inasemwa kwamba ni njia ambayo inadumu muda murefu bila kuchakaa hii ni
kwasababu hakuna kuchomeka chomoa kama njia nyingine (watumiaji wa chaja za
simu za iPhone watakubaliana na mimi jinsi chaja zetu zinavyochakaa).
Teknolojia hii pamoja na mazuri yake ukweli ni kwamba
teknolojia hii inatumia muda mrefu zaidi kuchaji kulinganisha na njia ya
kawaida, hii inasababisha watengenezaji wengi washauri kwamba watumiaji wa
chaja hizi kuchaji kwa mara ya kwanza kwa njia ya kawaida. Pia teknolojia hii
ya kuchaji kwa wireless inagharama kubwa kutengenezwa ukiringanisha na chaja za
kawaida. Kama ilivyo kwa kila teknolojia inakuwa na muungano wa wadau wa
teknolojia husika ambao unatengeneza viwango ambavyo ndio huongoza utengenezaji
wa vifaa vinavyotumiwa na teknolojia hiyo basi teknolojia hii ya chaja za
wireless inatawaliwa na miungano miwili mmoja ni ule wa Wireless Power
Consortium ambao unaungwa mkono na watengenezaji wa simu kama Nexus LG
Microsoft na HTC na muungano mwingine ni ule wa Power Matters Alliance ambao
wao wanaungwa mkono na kampuni la simu za mkononi ya AT&T ya nchini
Marekani.
SOURCE Pocketnow Website
>>Lengo langu ni kuakikisha upitwi na Habari za Teknolojia ungana Nami FACEBOOK , TWITTER na INSTGRAM