Mambo
vipi Rafiki? Naamini wengi wetu tunaamini simu zetu zikiingia maji basi
litakuwa tatizo lakini kwa jinsi Teknolojia inavyozidi kukua kila
kukicha, ndivyo tunavyozidi kupata vitu vya aina mbalimbali na vya
kustajabisha, kama simu hii ya kwanza
kutengenezwa ambayo inaweza kuoshwa na sabuni, simu hiyo iliyotengenezwa
na
kampuni ya kijapani ya KDDI simu hiyo inayo kwenda kwa jina la “Digno rafre”
inategemewa kuzinduliwa siku chache zijazo. Ndio zipo simu janja nyingi ambazo
zinauwezo wa kuzuia maji kuingia ndani ya simu lakini hii itakuwa ni simu ya
kwanza ambayo itaweza kusio tu kuzuia maji kuingia ndani bali hata kama utataka
kuiosha na sabuni basi utaweza kufanya hivyo bila kuwa na wasi wasi na
kuiharibu.
Simu hiyo inayotegemewa kuuzwa kwa karibu dola 175 za kimarekani
(Takribani laki nne za sh) na pengine itauzwa Japani tu kwa sasa. Watengenezaji
wa simu hii wanawalenga hasa wazazi ambao wanawatoto wadogo ambao ni rahisi
kuchafua simu zao. Simu hiii hata hivyo itaweza kuhimili kuoshwa na baadhi ya
sabuni sio kila sabuni, katika tangazo ambalo watengenezaji wa simu hiyo
wameliweka mtandaoni mtoto
anadondosha simu katika chakula na mama yake
anaonekana akiiosha katika bomba na sabuni kisha baadaye mtoto anaonekana
akichezea simu bafuni. Teknoloji inayotumika hapa ni ile ya kuzuia maji kuingia
ndani ya simu lakini imeongezwa pia uwezo wa kuzuia povu na sabuni, screen yake
kwa upande mwingine ni kwamba inaweza kutumiwa hata na mikono mibich
TAZAMA VIDEO HAPAReferences and useful resources:
>techlomedia
>>>Tafadhali Click link zifuhatazo kuhungana Nami FACEBOOK , TWITTER na INSTGRAM