Mara hii kampuni ya LG imeunda simu mpya aina ya LG V10 itakayokuwa na skrini mbili pamoja na kamera mbili kwa upande wa mbele.
Yafuatayo ni baadhi ya maelezo ya kiufundi yanayohusu simu ya LG V10;
- Skrini ya inchi 5.7 ya QuadHD Quantum IPS LCD
- Skrini ya pili ya inchi 2.1 yenye ubora wa 1040x160
- Teknolojia mpya ya kioo cha kulinda skrini aina ya Corning Gorilla Glass 4
- Kamera ya nyuma ya 16 MP f/1.8 LED na kamera nyingine mbili za 5 MP kwa upande wa mbele
- Uwezo wa kuchukuwa video za 4K
- Hifadhi ya 64 GB na MicroSD
- 4 GB RAM ile güçlü görünüyor.
- Uzito wa gramu 192
- Mfumo wa Android 5.1.1 Lollipop
- King’amuzi cha alama ya kidole
- Betri lenye uwezo wa 3000 mAh