Kwa mujibu wa maelezo yaliyotolewa na ShiftDelet.Net, kampuni hiyo imetangaza mpango wake wa kuingiza simu mpya aina ya Blackberry Priv zitakazotumia mfumo wa Android.
Mkurugenzi wa Blackberry John Chen alitoa maelezo kuhusiana na simu hizo mpya na kusema kwamba zinalenga kutimiza mahitaji ya watumiaji kikamilifu kutokana na muundo wa teknolojia ya hali ya juu.
Maelezo zaidi yanaarifu kwamba Blackberry Priv zitazinduliwa rasmi mwaka 2016 ingawa tarehe kamili ya uzinduzi haikubainishwa.