Computer ni
kifaa chenye kuhitaji matunzo na uangalizi wa hali ya juu,kwa kuwa itakapo
haribika huhitaji matengenezo ya gharama sana.Kuepukana na gharama hizi mmiliki
wa kifaa hiki anahitaja kufahamu njia sahihi za kutunza kifaa chake ili
kupelekea ufanisi wa kazi kwa hii computer pamoja na kudumu kwa muda mrefu.
Leo
tutaangalia njia ambalo unaweza ukazifuata kwenye computer yako na zikakuletea
matokeo ya haraka.Hazihitaji uwe na elimu kubwa sana ya computer bali uwe ni
mtumiaji wa computer inayotumia windows.
Tatizo
tutakaloliangalia leo ni ile hali ya computer kutumia muda mrefu kuwaka,kufanya
kazi taratibu,kusimama bila ya kufanya kazi (stuck) kabisa au hali zozote
zisizo za kawaida ambazo wengi wamekuwa
wakipoteza pesa zao kwa kupeleka computer kwa mafundi,mara nyingi maamuzi haya
yamepelekea kuleta matatizo ya kudumu kwenye computer.Tutaangalia mbinu pamoja
na vifaa (tools) vinavyopatikana ndani ya computer yako vinavyoweza
kukusafishia computer na kuirudisha katika ufanisi wake.
Kwa
watumiaji wa windows kuna tools ambazo zinaweza kukusaidia katita matatizo
madogo madogo yanayohusu utunzaji wa computer.Kuna tools ambazo unaweza ukashusha(download)
na kuzitumia kama vifaa vya kusafishia computer yako
Disk cleanup
Hii hutumika
kwenye windows zote ni njia rahisi na haraka ya kusafishia kifaa cha kutunza
data zako katika computer (Hard Disk).
Drive Optimizer
Task Manager
Hii ni njia
ya kuchunguza ufanisi wa computer katika tatizo la computer kufanya kazi
taratibu kupita kiasi
File History
Tunza
taarifa (data) zako kuzikinga na upotevu wa aina yoyote ule.File History na
System image zinakuwezesha kutunza (Backup) taarifa.
Njia
nyingine ambazo unaweza kutumia katika kuitunza computer yako ni kutumia
programs za bure(Free Download) zitakazo kusaidia kusafisha na kutunza Data
zako hewani(cloud storage) ni System Cleaners na Free cloud storage.
Cloud Storage
Google
Drive(15GB) na Microsoft OneDrive(7GB), hizi ni njia rahisi za kuhifadhi Data
zako hewani na kuzitumia mudfa wowote utakao zihitaji.
Kwa
utangulizi tumeona njia rahisi za kutumia ili computer yako iendelee kuwa na
ufanisi wa hali ya juu.
Kupitia
vielekezi(link) vilivyowekwa katika kila njia utaona namna ya kutumia njia moja
baada ya nyingine.