Mitandao ya kijamii imezidi kupanuka kwa karne ya sasa ya teknolojia ya habari,mabilioni ya watu wameunganishwa kupitia mitandao hii kama twitter,facebook na mingine mingi.Watu wamekuwa wakishirikishana katika mambo mbalimbali yanayowazunguka kila siku.
Katika mitandao hii ya kijamii watu wanapokuwa wanapendelea jambo fulani hujiunga na kutengeneza mijadala na mazungumzo ya mara kwa mara kuhusiana na jambo hilo.Kupitia mijadala hii ndio tunapata masoko kupitia mitandao ya kijamii(social media marketing).
Watu wanapokuwa wanazungumzia bidhaa au
huduma fulani kupitia mitandao ya kijamii inapelekea bidhaa au huduma
hii kusambaa kwa haraka sana katika midomo ya watu.
Ubora na thamani ya bidhaa hiyo ndio
utakao pelekea umaarufu wa hali ya juu ndani ya mitandao hiyo,kwa maana
hii bidhaa hii itakuwa ni yenye kutafutwa kwa hali ya juu na kupelekea
ongezeko la wateja katika bidhaa hiyo.
Ijapokuwa kwa upande wa pili pia ikiwa
bidhaa itaongelewa vibaya katika mitandao hii watu watashawishika
kuikimbia na kusababisha kudorora kwa bidhaa hii.
Katika mitandao ya kijamii watu wanaweza kutengeneza makundi maalum kuzungumzia jambo fulani ambalo litawakusanya wapenzi ya jambo hilo katika kundi moja,hapa ndipo soko linapotengenezwa.
Katika mitandao ya kijamii watu wanaweza kutengeneza makundi maalum kuzungumzia jambo fulani ambalo litawakusanya wapenzi ya jambo hilo katika kundi moja,hapa ndipo soko linapotengenezwa.
Ikiwa mtu ni mfanyabiashara wa computer na vifaa vya teknolojia anaweza akapata soko la bidhaa zake ikiwa atatembelea makundi katika mitandao ya kijamii yanayozungumzia computer na teknolojia.Hii itamsaidia kufikia wateja wake kwa urahisi zaidi.
Dhana ya biashara kupitia mitandao ya kijamii imeonesha mafanikio makubwa kwa baadhii ya biashara kwa kuwa zimefuata kanuni ndani yake.
Kanuni ya biashara kupitia mitandao ya kijamii ni kuelezea bidhaa yako kwa makundi husika,kueleza biashara kwa ubora wake halisi,kuelezea biashara mara kwa mara na mwisho ni kutoa huduma kwa namna ulivyoitangaza.Kinyume na kanuna hii kutapelekea kusambaa kwa sifa mbaya juu ya biashara hiyo.
Kupitia dhana hii kumekuwa na ongezea la makampuni yanayojihusisha na kutangaza bidhaa na huduma yao katika mitandao ya kijamii kwa kuwa kuna ongezeko kubwa la vizazi vinavyojisajili katika mitandao hii.Hii ni nafasi ya kutangaza bidhaa zako katika mitandao ya kijamii na kuongeza mtandao wa wateja wako.
Endelea kutembelea mara kwa mara katika kurasa wetu wa social media ili uweze kupata elimu zaidi juu ya njia hii ya biashara.
Mshirikishe mwenzako katika mtandao wako wa kijamii kwa kubonyeza kitufe cha share hapa chini.
Mshirikishe mwenzako katika mtandao wako wa kijamii kwa kubonyeza kitufe cha share hapa chini.