Youtube ni tovuti maarufu sana duniani inayojihusisha na masuala ya kushare videos, ni mahali ambapo unawez
a
kupata si tu videos za muziki na burudani bali pamoja na videos za
kuelimisha na kujifunza masuala mbalimbali. Mara nyingi watumiaji wa
Youtube hupenda kupakua (download) videos zinazowavutia kwa matumizi ya
baadaye, lakini Youtube haina uwezo (feature) hii "by default".
Pia kwa wale wanaotumia browser kama Chrome pamoja na
variants zake wanaweza kuweka
extensions zenye kufanya kazi hiyo (Youtube/Video Downloaders) ambazo zinapatikana kwa wingi katika store ya Chrome inayojulikana kama
Chrome WebStore. Lakini pia ili kufanikisha mchakato wa kupakua videos hasa zilizopo Youtube kuwa rahisi zaidi unaweza kutumia browsers kama
Baidu Browser au
Spark Security Browser ambazo zimetengenezwa
zikiwa na uwezo wa ndani (built-in capability) wa kupakua video kutoka
katika tovuti kama Youtube, hauhitaji extension wala programu yoyote
kuwezesha hilo, browser husika ndiyo ina uwezo huo.
Kwa wale wanaotumia smartphone (Android) kutembelea Youtube, si rahisi
kupakua video hizo! si tu kwa kutumia browser ya simu, bali hata kwa
app rasmi ya Youtube inayopatikana Google PlayStore. Lakini kwa kutumia app inayoitwa OGYoutube suala hili si gumu tena. OGYoutube ni modded app(
modding ni muongezo au boresho la software ili iweze kufanya kazi zaidi ya vile inavyopaswa) inayokuwezesha
kupakua video kutoka Youtube moja moja katika smartphone yako. Kifupi
ni app ya Youtube iliyoongezewa uwezo (features).
Features za OGYoutube
1. Pakua (Download) video zaidi ya moja kwa muda mmoja.
2. Angalia na download video katika ubora (video quality) wowote unayotaka, kuanzia 144p hadi 1440p
 |
Download |
 |
Ubora wa Video |
3. Pakua Subtitle za video husika.
4. Popup Player, angalia video huku ukiwa unaendelea kutumia simu kwa kufanya mambo mengine.
 |
Subtitle |
 |
Popup Player |
5. Pakua video ikiwa katika mfumo wa sauti tu (MP3).
6. Pia unaweza angalia video hata screen yako ikiwa katika lock.
Downloads
Link: Download OGYoutube
HAPA OGYoutube v0.9
Official Webiste:
OGMods
Kumbuka
1. Ili kuinstall app hii, lazima uwe umeruhusu simu yako kuweza
kuinstall apps kutoka katika vyanzo visivyo rasmi (unknown sources)
Kama bado, Ingia katika "
Settings" ya simu yako, kisha nenda katika "
Security". Ndani ya security tafuta mahala palipoandikwa "
unknown sources", hakikisha sehemu hii ipo
activated.
2. Baada ya kuinstall itatengeneza shortcuts mbili, ya kwanza ndiyo app
yenyewe (OGYoutube), na ya pili ni shortcut yenye jina la
Downloads, ambayo
itahifadhi videos unazopakua kutoka Youtube.