Ushawahi kusikia mtu ameharibu kioo chale cha laptop kwa sababu tuu alikuwa anakisafisha? Kama bado ufahamu uwe inatokea, na sababu kubwa inakuwa ni utumiaji wa njia ambazo si salama kwa vioo (display) vya teknolojia ya LCD.
Hatua ya kwanza:
Zima kifaa chako, iwe laptop au TV yako.
Na kwa usalama zaidi chomoa waya kutoka kwenye umeme kabisa, kwa
laptop ikiwezekana chomoa betri – kama imeshindikana hakikisha ulichagua
'Shutdown' na wala si 'Hibernate' au 'Sleep'.
Hatua ya pili:
Umeme na unyevu nyevu havipatana, hakikisha umezima kabisa kifaa
chako.
Tafuta kitambaa laini na nyororo, ushauri bora kama ukipata vile
vitambaa spesheli kwa ajili ya kusafishia miwani basi ndio zitafaa zaidi. Alafu
kilainishe kidogo, kumbuka ni kulainisha kiduchu tu….na si kukiloweka kwenye
maji. Kitambaa kinatakiwa kisiwe na mimaji maji, maji kidogo ni kwa ajili ya
kukifanya kiwe laini zaidi.
