Gari ya Apple Car iliyokuwa ikifanyiwa majaribio kwa muda mrefu, inatarajiwa kuingizwa rasmi barabarani mwaka 2019.
Gari hiyo iliyoundwa katika mradi wa Titan unaojumuisha wahandisi 600 wenye utaalamu wa hali ya juu, inatarajiwa kuvutia wengi kwa muundo wake wa teknolojia ya kisasa.
Ingawa Apple Car inaarifiwa kutumia umeme, bado haijabainishwa iwapo itaendeshwa na dereva au itaweza kujidhibiti yenyewe.
Vyanzo vya karibu vya kampuni hiyo pia vimefahamisha kwamba Apple Car itakuwa na usukani.