Kampuni kubwa ya mtandao wa jamii wa Facebook imearifiwa kuleta maboresho ya muonekano wa kurasa yake katika vifaa vinavyoendeshwa kwa mfumo wa iOS.
Kuaniza sasa watumiaji wa vifaa vinavyoendeshwa kwa mfumo wa iOS, watakumbana ana kwa ana na muonekano mpya wa kurasa ya Facebook watakapofungua.
Miongoni mwa maboresho yaliyofanyika ni kubadilishwa kwa muonekano wa logo ya Facebook inayovutia zaidi kuliko ya zamani.
Vile vile kuna sehemu nyingine ndogo ndogo za picha zilizofanyiwa mabadiliko.