Google tayari wamefika mbali kabisa katika teknolojia ya utengenezaji wa magari yanayojiendesha yenyewe na sasa Apple pia wamejitupa katika teknolojia hiyo hiyo.
Uhakika
mkubwa juu ya kampuni ya Apple kujiingiza kwenye suala la utengenezaji
wa magari umejulikana baada ya injinia mmoja wa kampuni huyo kwenda
kuomba kibali cha kutumia uwanja mmoja wenye barabara kadhaa nchini
Marekani kwa ajili ya majaribio ya magari hayo.
Kampuni
ya Google (kwa sasa ALPHABET) tayari imefika mbali zaidi katika
teknolojia ya magari yanayojiendesha yenyewe na inaonekana Apple pia
imeamua kutoachwa nyuma katika hili. Wengi wanaona teknolojia ya namna
hii (magari ya kujiendesha yenyewe) itakuwa kubwa sana miaka michache
baadae. Na kikubwa zaidi wote, Google na Apple, wanaamini kuna umuhimu
mkubwa wa vifaa kama simu na tableti kuweza kuwasiliana moja kwa moja na
gari lako. Fikiria uingie kwenye gari na uweze kutumia huduma mbali
mbali za simu yako bila kushika simu hiyo.