Header ads

Header ads
» » Ronaldinho arejea nyumbani; ajiunga na Fluminense

 Ronaldinho arejea nyumbani; ajiunga na Fluminense

Mchezaji maarufu wa Brazil, kipenzi cha mashabiki wa kabumbu na mshindi wa taji la Ballon d'Or Ronaldinho arejea Brazil

Ronaldinho ambaye alikuwa amesemekana kuelekea timu ya Antalya Spor ya Uturuki, ameamua kubaki Brazil baada ya kuingia mkataba na timu ya Fluminense.
Fluminense ilitangaza habari hii kupitia mtandao wa kijamii wa twitter ambapo walisambaza picha za Ronaldinho akiwa na jezi nambari kumi ya timu hiyo.
Ronaldinho alisalia bila timu baada ya kuondoka kutoka kilabu cha Queretaro cha Meksiko mwezi uliopita.
Mkongwe huyu wa Brazil anakumbukwa sana kutokana na mchango wake katika timu ya taifa ya Brazil iliyotwaa kombe la dunia mwaka wa 2002 na pia kwa kipindi chake akiwa na Barcelona.
Ronaldinho alianza soka katika timu ya Gremio kabla ya kuchezea PSG, Barcelona na AC Milan.

Imehaririwa na;- poatel Africa

Habari yako! Endelea kutembelea Tovuti ya TeknoTaarifa kwa Taarifa murwa za Teknolojia kutoka ndani na nje ya Tanzania, Tupo kwa ajili ya wapenzi wa Teknolojia.
«
Next
PICHA:: Taarifa za kuvamiwa kwa kituo cha Polisi STAKISHARI Jijini Dar  Watu waliokisiwa kuwa majambazi wamekivamia kituo cha polisi Stakishari ukonga.  Kwa mujibu wa taarifa za awali watu hao inasemekanaya wamevunja store ya  silaha na kuchukua silaha zote aina ya SMG zilizopo kituoni hapo….hadi sasa inasemekana kuna vifo vya polisi  ambao idadi yake haijajulikana wameuwawa  na pia kuna  jambazi mmoja aliyepigwa na risasi ya jambazi mwenzie….Jambazi huyo aliyeuwawa inasemekana ni dereva wa bodaboda wa kituo cha Nji Panda aliyefahamika kwa jina la Madevu.  
»
Previous
UKAWA nao kumtangaza mgombea wao Jumanne ijayo.