Home
»
MICHEZO
» John Bocco Akataa Kujiunga na Free States ya Afrika Kusini...Nafasi yake Imechukuliwa na Huyu
MSHAMBULIAJI Frank Kalanda wa Uganda iliyoitoa Tanzania katika Raundi ya Kwanza kufuzu CHAN ya mwakani, amechukua nafasi ya John Raphael Bocco klabu ya Free State Stars ya Afrika Kusini.
Azam FC ilikubali kumuuza mshambuliaji wake John Raphael Bocco ‘Adebayor’ kwa dola za Kimarekani 80,000 zaidi ya Sh. Milioni 160,000 za Tanzania kwa klabu ya Free State Stars, lakini mchezaji huyo ‘akazingua’.
Mrisho Khalfan Ngassa aliyesajiliwa na Free State Mei mwaka huu kutoka Yanga SC, ndiye aliyemuunganishia Bocco dili la kujiunga na timu hiyo ya Ligi Kuu ya ABSA.
Mazungumzo baina ya FS na Bocco yalifanyika vizuri na mshambuliaji wa Tanzania mwishowe akawaambia Azam FC; “Ninabaki hapa hapa, siendi popote, mimi bado”.
Kalanda kulia akiwa na Mrisho Ngassa kwenye la FS kwa safari la Johannesburg kuweka kambi
FS ilimpa mshahara mzuri Bocco, mara mbili ya ule anaopata Azam FC kwa sasa, lakini haikutosha kumshawishi mshambuliaji mrefu ahamie Bethlehem, ndipo ikaamua kuhamia kwa Kalanda aliyechangamkia dili ‘chap chap’.
Tayari Kalanda yupo kambini na FS katika hoteli ya Lake View mjini Johannesburg kujiandaa na Ligi Kuu ya Afrika Kusini, inayotarajiwa kuanza Agosti 8, mwaka huu.
Timu hiyo ya kocha Mmalawi, Patrick Phiri inatarajiwa kuanza na Black Aces, wakati mechi ya pili watacheza na mabingwa watetezi, Kaizer Chiefs. Mechi ya kwanza, Kaizer wataanza kutetea taji lao dhidi ya Chippa United Agosti 8.
Kwa mujibu wa ratiba ya msimu wa PSL wa 2015-16, Mamelodi Sundowns wataanza na Platinum Stars, Orlando Pirates na SuperSport United, wakati timu mbili zilizopanda msimu huu, Golden Arrows na Jomo Cosmos watakuwa nyumbani na University ya Pretoria na ugenini na Maritzburg United.
Kalanda anayetokea URA ya kwao, ametua kwa bei rahisi Bethlehem na mshahara nafuu kuliko ambao FS ingetoa kwa Bocco.
Tanzania, Taifa Stars baada ya kufungwa 3-0 na Uganda katika mchezo wa kwanza Zanzibar ilimfukuza aliyekuwa kocha wake Mholanzi, Mart Nooij na timu hiyo kukabidhiwa kwa mzalendo, Charles Boniface Mkwasa ambaye alikwenda kutoa sare ya 1-1 na Uganda katika mchezo wa marudiano mjini Kampala.
John Bocco amekataa kujiunga na FS, nafasi ambayo imechukuliwa na Mganda Sekisambu
Topics: MICHEZO
Imehaririwa na;- Unknown

Habari yako! Endelea kutembelea Tovuti ya TeknoTaarifa kwa Taarifa murwa za Teknolojia kutoka ndani na nje ya Tanzania, Tupo kwa ajili ya wapenzi wa Teknolojia.
Soma na Hizi
Bayern Munich kutoa msaada wa kifedha kwa ajili ya wahamiaji nchini Ujerumani
Mabingwa wa Bundesliga kufungua kambi ya mazoezi na kutoa msaada wa k...Read more »
05Sep2015Michezo ya Commonwealth 2022 kufanyika barani Afrika
Durban itakuwa mji wa kwanza ...Read more »
03Sep2015Nyota wa Barcelona Lionel Messi aondoka na tuzo mbili za UEFA
Mshambuliaji matata wa Barcelon...Read more »
29Aug2015Mshambuliaji mwingine kutoka Mali atua Simba kwa majaribio
MSHAMBULIAJI Makan Dembele kutoka Mali amewasili nchini kwa majaribio ya kujiunga na Simba ...Read more »
27Aug2015AZAM TV na FERWAFA zasaini mkataba wa kitita cha dola bilioni 2,35 za kimarekani
...Read more »
25Aug2015Bolt aendelea kutawala mbio za mita 100 Beijing
...Read more »
24Aug2015

Playstore
TeknoTaarifa Video
TAARIFA ZILIZOSOMWA SANA
-
Computer ina uwezo wa kufanya mambo ambayo binadamu...
-
Mambo vipi Rafiki yangu? Kama wewe ni miongoni mwa...
-
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala...
-
BEST TANZANIAN UNIVERSITIES 2015: Latest Rankings ...
-
Coca-Cola Kwanza Limited of Dar es Salaam, is part...
-
Kampuni ya Samsung Electronics Co Ltd imeanza...
-
Kwa wale Rafiki zangu wa ma-gadgets and all...
-
Si wengi wetu wanaofahamu umuhimu wa kula samaki mara...
Data Boosta
