Header ads

Header ads
» » Zidane aomba kurejeshewa jezi yake ya mwaka 1998

 Zidane aomba kurejeshewa jezi yake ya mwaka 1998

Nyota na shujaa wa kombe la dunia la FIFA mwaka 1998, Zinedine Zidane huenda anataraji kurejeshewa jezi yake ya mwaka 1998

Julai 12 mwaka 1998 Ufaransa, timu ya kabumbu ya Ufaransa iliwafurahisha mashabiki wake kwa kuichabanga mabao matatu kwa nunge timu ya Brazil na kuchukuwa kombe la dunia mwaka huo.
Mabao mawili yaliosawazishwa na Zinedine Zidane katika kipindi cha kwanzo, na bao la 3 yalipelekea ushindi wa timu hiyo jambo ambalo lilisababisha nyota huyo kukumbwa na furaha isiokuwa na kifani na kuwarushia mashabiki wake jezi yake maarufu namba 10 mgongoni.
Miaka 17 baada ya tukio hilo, Zinedine Zidane alifahamisha katika kituo cha habari cha RTL Jumapili kuwa anasikitika kuwarushia mashabiki wake jezi hilo.
Ikiwa shabiki wa Ufaransa aliebahatika kupokea jezi hilo atasikia wito huo, je? Atarejesha jezi hilo kwa Zidane?
Ingekuwa wewe ungefanyaje?

Imehaririwa na;- poatel Africa

Habari yako! Endelea kutembelea Tovuti ya TeknoTaarifa kwa Taarifa murwa za Teknolojia kutoka ndani na nje ya Tanzania, Tupo kwa ajili ya wapenzi wa Teknolojia.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post