Gavana wa New York, Andrew Cuomo ameeleza kuwa hiyo ni mara ya kwanza kwa kipindi cha miaka 150. Wafungwa hao wawili walikua katika vyumba vinavyokaribiana na wakachimba tobo ukutani na kutambaa na kutorokea nje.
Jamaa hao waliweka nguo vitandani mwao ili kuonyesha kuwa walikua wamelala, na ilipofika asubuhi ndipo ikagundulika kuwa wameshaondoka.
Aidha wafungwa hao walitambulika kwa majina kama David Sweet na Richard Matt. David Sweet mwenye umri wa miaka 34 alihukumiwa kifungo cha maisha mnamo baada ya kumuua msaidizi wa afisa usalama mnamo mwaka 2002.
Naye Richard Matt mwenye umri wa miaka 48 alikua anatumikia kifungo cha miaka 25 jela kwa makosa ya mauaji, unyang'anyi na utekaji nyara.
Utorokaji huo unafananishwa na filam ya "The Shawshank Redemption," iliyoigizwa mwaka 1994.
Operesheni kabambe ya kuwasaka wafungwa hao immeanzishwa huku mamia ya askari wakiwa wamesambazwa mtaani kuwasaka wakali hao.