Baadhi ya wafanyabiashara wanatuhumiwa kuugeuza mwezi wa Ramadhan kuwa, ndio wa kuchuma zaidi kibiashara kwa kupandisha bei za bidhaa, zikiwemo viazi vitamu, mihogo, maharage, magimbi na tambi ambavyo hutumiwa na wengi.
hali hii inawafanya wananchi wengi hasa wenye kipato kidogo washindwe kumudu bei za vyakula wanapokwenda sokoni.
Hili niombi langu kwa Wafanyabiashara husika,nawaomba muache tabia hii kwani sio nzuri hata mbele za Mungu.
Niwatakie mfungo mwema wa mwezi Mtukufu wa Ramadhan