Rais Barak Obama amesema mauaji ya
watu tisa ndani ya Kanisa la Waafrika Wamarekani katika eneo la
Charleston katika jimbo la Carolina Kusini yanaibua maswali kuhusu
sehemu mbaya ya historia ya Marekani.
Katika hotuba yake
iliyoonyeshwa katika televisheni muda mfupi baada ya polisi kumkamata
mtuhumiwa ambaye ni kijana wa kizungu-- Bwana Obama amesema chuki
miongoni mwa jamii kwa misingi ya rangi na imani ni kitisho kwa
demokrasia ya Marekani na misingi yake.Amesema mauaji ya watu wengi hayatokei kwa kiasi hiki katika nchi nyingine zilizoendelea, na ametaka kufanyika kwa mabadiliko ya pamoja katika fikra za Wamarekani kuhusu ghasia zinazosababishwa na matumizi ya silaha.