
Mwanariadha
wa Marekani, Justin Gatlin amevunja rekodi iliyowekwa na Usain Bolt na
kuweka rekodi mpya katika mbio za Diamond League za mita 100.
Gatlin
mwenye umri wa miaka 33 anayeishi huko Orlando, Florida, aliwaongoza
wenzake kushinda kwa sekunde 9.75 ikiwa ni muda bora wa saba kuwekwa
katika historia na ameipiku rekodi ya Bolt (lightning Bolt) ya sekunde
9.76 iliyoweka mwaka wa 2012.
Gatlin
ambaye amepigwa marufuku kutumia dawa za kusisimua misuli alikimbia mda
wa sekunde 9.74 katika mkutano wa kwanza wa mbio za Diamond League
mwezi uliopita.
Bingwa
wa mbio za Olimpiki Sally Pearson alipata jeraha la kifundo cha mkono
baada ya kuanguka katika mbio za kuruka viunzi za mita 100 upande wa
wanawake.