Header ads

Header ads
» » Hili Ndilo Kabila Wanaojikata Vidole Kila wanapofiwa kama Njia ya Kuomboleza Kifo

 kidole
Dunia ina vituko vya kila aina, ukistaajabu ya Musa utayaona ya firauni!
Huzuni au kufiliwa na mtu ni pigo kubwa sana, hasa awe ni rafiki azizi, mmoja wa familia, mumeo/mkeo au wanao wapendwa.  Kila dini, kila jamii zina njia zake za kuhuzunika wakati wa kifo.  Hatahivyo, mengine ni ya kustaajabisha.
Sasa vituko viko hapa! Kuna jamii moja inaitwa ‘Dani’ ilioko katika kisiwa cha Papua New Guinea kiliopo karibu na Indonesia. Jamii hii ina njia ya kipekee ya kuonyesha huzuni yao kwa mtu wao. Jamii hii kila ikipata msiba wa mmoja wao kufariki basi watu hawa (hususan wanawake) wanakata kidole kimoja kama ishara ya kuondokewa na mpendwa wao. Na wanaanza na kidole kirefu, isipokuwa mzazi akifiwa na mwanaye mchanga anaanza kukata kidole kidogo!
dani1
Itikadi yao ni kuwa hivyo vidole vinaashiria nambari ya familia ya kila mmoja. Sasa iwapo mmoja atakufa basi hutumia jiwe kali au kisu kukata kidole karibu na kaburi. Kidole hicho huwekwa juu ya kaburi kwa masiku mpaka kinyauke, alafu kinachomwa mpaka kuwa majivu na kurushwa juu ya kaburi. Basi hapo huwa mizimu wa waliokufa hayawafikii majumbani mwao, naye aliyekufa huwa radhi pale alipolala!

Imehaririwa na;- poatel Africa

Habari yako! Endelea kutembelea Tovuti ya TeknoTaarifa kwa Taarifa murwa za Teknolojia kutoka ndani na nje ya Tanzania, Tupo kwa ajili ya wapenzi wa Teknolojia.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post