Mchezaji wa Chile Gonzalo Jara, aligonga vichwa vya habari baada ya kumgusa makalio mshambuliaji wa Uruguay Edison Cavani katika mechi ya robo fainali.
Uongozi wa Copa America umechukuwa uamuzi wa kumfungia Gonzalo Jara kucheza mechi za Copa America kutokana na kitendo hicho cha aibu.
Nyota wa Uruguay Edison Cavani alipandwa na midadi na kumfokea refa baada ya kuonyeshwa kadi nyekundu licha ya kufanyiwa uhuni na Jara.
Licha ya wenyeji wa maandalizi wa mashindano hayo Chile kufuzu katika hatua ya nusu fainali, watakosa huduma ya Gonzalo Jara aliyepewa adhabu na uongozi wa Copa America.