Katika Gazeti la Mwananchi la Leo hii kuwa Kiongozi Mkuu wa ACT-Wazalendo Zitto Zubeir Kabwe na Mwenyekiti wake Anna Mgwira wameshindwa kumaliza mikutano yao kadhaa Mkoani Geita baada ya kuzomewa nawananchi.
Gazeti hilo limeandika katika moja ya kurasa zake za ndanikuwa Zitto katika mkutano wake wa kwanza uliofanyika nje ya Mji wa geita,alishindwa kuhutubia baada ya wananchi kumtaka aeleze kwanini alifukuzwa Chadema na kwanini anataka wananchi waendelee kumwamini licha ya kuonekanaMsaliti? Zitto na mwenyekiti wake walishindwa kuendelea kuhutubia na hivyomkutano Kuvunjika.
Kisha wakaelekea Geita Stand kufanya mkutano wa hadhara. Mwenyekiti alianza kukumbwa na zomeazomea wananchi wakitaka ashuke jukwaani kumpisha Zittopeke yake. Mwenyekiti akashuka kisha Zitto akapanda jukwani. Alipoanza kuhutubiaZitto akajifananisha na ng’ombe kwa kudai kuwa siku zote ng’ombe huwahatikisiki bali mkia ndio unaotikisika. Kisha akasema yeye ni sawa na ng’ombena chama alichokihama (Chadema) ni sawa na mkia.
Kauli hiyo ikaamsha hasira za wananchi na kuanza kumzomeaZitto kwa kuikashifu Chadema na kumuita kuwa yeye ni Msaliti na ndio sababu alitimuliwa na Chadema. Jitihada za Zitto kutuliza umati wa wanageita haizikufanikiwa na hivyo kumfanya Zitto ashuke jukwaani na kumaliza mkuano hapohapo bila kupenda.
Ajabu, Gazeti la Mwananchi limeandika habari hii katikati ukurasa wa ndani karibu na mwisho kabisa huku magazeti mengine yasiandike kabisa kasheshe hii. Ikumbukwe kuwa wakati wa ziara za mwanzo za ACT, magazeti karibu yote yalikuwa yakizipa habari za Zitto umuhimu wa juu kaika kurasa zamwanzo. Leo hayaandiki tena labd akwa kuwa ni habari mbaya kwa ACT Wazalendo na Zitto mwenyewe.
Watu wamemchoka Zitto au ni kwamba ukweli umeanza kudhihirika? Yetu macho.