Hii imekua stori kubwa sana ndani ya masaa machache kutokana na watu wanaosambaza habari zisizo na ukweli kuwa msanii Banza Stoni amefariki dunia
Si Mara ya kwanza kwa banza kuzushiwa kifo amesema mwenyewe "Walianza kunizushia nimekufa tangu mda mrefu naweza sema sasa hii Mara ya mia (100) sijui ni nani huyo asiyekuwa na haya jamani"
Banza pia aliongezea kwa kusema "Mimi nilikua naumwa tuu Ila kwa sasa mzima naendelea na dozi zangu , marehemu anaongea tena, marehemu anakula na kuendelea tena kuishi , basi marehemu Mimi wa aina nyingine, kila kukicha nazushiwa kifo "
Kwa habari nyingi nyingne endelea kubaki hapa hapa utazipata zote mshirikshe na mwingine azipate hizi