Apple imetangaza kwamba itatoa huduma kwa wasikilizaji wa muziki watakaoweza kujiunga na Apple Music kwa malipo ya fedha dola 9.90 kwa mwezi.
Wakati huo huo, Apple pia imebainisha fedha watazolipwa wanamuziki. Kwa mujibu wa hesabu zilizofanywa, mwanamuziki ataweza kulipwa fedha dola 20,000 kwa kila nyimbo itakayosikilizwa mara milioni 1 kwenye Apple Music.
Mradi huu wa Apple Music unatarajiwa kuimarisha biashara katika sekta ya muziki na kuwasaidia wasanii kufaidika wanapoweka nyimbo zao mitandaoni.