Header ads

Header ads

headlines

» » Vifaa vya uchaguzi vyachomwa moto Burundi

 Vifaa vya uchaguzi vyachomwa moto Burundi

Vifaa vya uchaguzi vyachomwa moto mkoani Kirundo kaskazini mashariki mwa Burundi

Watu waliobebelea silaha walivamia kituo kimoja kilichokuwa kimehifadhiwa vifaa vya uchaguzi unaotarajiwa kufanyika Jumatatu nchini Burundi.
Shambulio hilo lilifanyika usiku wa Ijumaa ambapo masanduku 59 yameripotiwa kuchomwa moto na watu hao.
Kwa mujibu wa taarifa iliotolewa na mwenyekiti wa wilaya, Marineau Hitimana alifahamisha kuwa mapambano bain aya watu hao na askari Polisi ilichukuwa muda wa dakika takriban 10.
Hitimana alifahamisha kuwa ilibidi kutuma kikosi cha wanajeshi kufaulu kusitisha shambulio hilo.
Shambulio hilo limetokea kipindi ambapo kumesalia siku 2 ili uchaguzi wa wabunge na madiwani ufanyike.

Imehaririwa na;- poatel Africa

Habari yako! Endelea kutembelea Tovuti ya TeknoTaarifa kwa Taarifa murwa za Teknolojia kutoka ndani na nje ya Tanzania, Tupo kwa ajili ya wapenzi wa Teknolojia.
«
Next
NEC yaahirisha uandikishaji kwa BVR Dar es salaam
»
Previous
Apple Music wamejipanga kuwasaidia wasanii katika bishara ya muziki