Meneja wa Samatta, Jamal Kisongo amesisitiza kwamba lazima mshambuliaji huyo Mtanzania ataondoka na kucheza Ulaya.
“Hata uongozi wa Mazembe nimeishazungumza nao, lazima Mbwana ataondoka msimu huu. Atarudi tena CSKA kufanya mazoezi na kuangalia nini kitafuatia.
“Unajua wakati ule alipata maumivu ya enka, hakuweza kumalizia majaribio. Lakini kipande cha majaribio alichofanya, kilikuwa na mafanikio makubwa.
“Hivyo TP Mazembe wameishakubali kwamba watamuachia tena akafanye majaribio,” alisema Kisongo.
Samatta anatumikia mwaka wa mwisho wa mkataba wake na Mazembe na ikishindwa kumuuza sasa, inaweza kumpoteza kama ataondoka na yenyewe haitapata kitu.
Samatta amekuwa tegemeo la ushambuliaji katika kikosi cha Mazembe hasa baada ya kuondoka kwa Tresor Mputu.