Header ads

Header ads
» » Hii Ndiyo Taarifa ya RAY na DAVINA Kuhusu kutaka Kuchapana Makonde Ukumbini


Mastaa wa Bongo Movies, Vincent Kigosi ‘Ray’ na Halima Yahaya ‘Davina’ nusura wazichape kavukavu katika Ukumbi wa Mlimani City, jijini Dar baada ya Ray kudaiwa kumshika mwenzake huyo sehemu nyeti, Risasi Mchanganyiko lina mchapo kamili.

Kwa mujibu wa chanzo makini cha gazeti la Risasi, ambacho kilikuwa shuhuda wa tukio hilo, Davina alikuwa amekaa na wasanii wengine pamoja na Mlezi wa Bongo Movies, mama Loraa wakipata vinywaji ndipo Ray alipofika na kuharibu shughuli.


“Wakati Davina anaendelea kupata kinywaji na mama Loraa, alitokea Ray akiwa tayari ‘ameshakula vyombo’ na kumshika Davina kalio kitendo kilishomkasirisha sana msanii huyo na kuanza kumcharukia Ray,” kilisema chanzo hicho na kuongeza:

“Davina alinyanyua glasi ya kinywaji chake, akammwagia Ray huku akimuuliza kwa nini alimshika makalio ndipo Ray naye alipopandisha hadi wakataka kukunjana.”
Baada ya vurugu hizo kuanza kushika kasi, alitokea mwigizaji Steven Mengere ‘Steve Nyerere’ na wenzake ambao waliwasihi wawili hao waachane na mambo hayo.


Baada  ya kupata habari hiyo, gazeti hilo liliwatafuta wahusika ambapo lilianza na Davina.
“Jamani mi nafikiri nisizungumzie hilo tukio maana naona ni la aibu, si kitendo kizuri na kinaniumiza mno kwa maana ni udhalilishaji mno na kwa nini mtu akufanyie hivyo?,” alisema Davina. Simu ya Ray iliita bila kupokelewa.

Imehaririwa na;- poatel Africa

Habari yako! Endelea kutembelea Tovuti ya TeknoTaarifa kwa Taarifa murwa za Teknolojia kutoka ndani na nje ya Tanzania, Tupo kwa ajili ya wapenzi wa Teknolojia.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post