Profesa mmoja aliyekuwa
akiwasilisha mada katika chuo kikuu cha Wageningen huko Uholanzi,
amejikuta katika fedheha ya aina yake mbele ya wanafunzi aliokuwa
akiwafundisha baada ya mashine ya kuonyeshea picha (projector) iliyokuwa
kwenye ukumbi aliokuwa akifundishia kumuumbua alipokuwa akiangalia
picha za ngono.
Profesa huyo ambaye vyombo vya habari
vya Uholanzi vimeamua kutolitaja jina lake, alikuwa akifundisha
wanafunzi hao kwa kutumia kifaa hicho kilichokuwa kimeunganishwa na
kuonyesha somo lake kutokea kwenye laptop yake, na alipomaliza akasahau
kuchomoa waya za kuunganisha vifaa hivyo viwili ili aendelee na mambo
yake.
Kufuatia hali hiyo, huku akiwa hajui
kama wanafunzi wake walikuwa wakifuatilia alichokuwa akikifanya, profesa
huyo ambaye anatajwa kuwa ni mtu mzima kidogo kiumri, aliingia kwenye
mtandao wa internet na kuanza kufungua site mbalimbali, huku wanafunzi
wake wakiwa wanaangalia na kuona alichokuwa akikifanya kupitia projector
ya ukumbini hapo.
Lakini wanafunzi hao sio tu kuwa
waliendelea kumshangaa profesa huyo, bali mmoja wao alikwenda mbali
zaidi kwa kupiga picha na kuipost kwenye mtandao wa kijamii muda huo
huo, hali ambayo ilileta tafrani ya aina yake.
Haijajulikana hadi sasa kama profesa
huyo atachukuliwa hatua au laa, na ikiwa atachukuliwa hatua, kuwa ni
hatua gani zitakazochukuliwa dhidi yake, lakini ni wazi kuwa, tukio hilo
litakuwa limemfedhehesha vya kutosha sana.