Header ads

Header ads
» » Mwanasheria aeleza jinsi sheria ya makosa ya mtandaoni itakavyowapeleka jela wanaopenda kutukana Instagram


Mwanasheria maarufu nchini, Alberto Msando amesema sheria mpya ya makosa ya mtandaoni itakula kwa wengi.

Msando ameiambia Bongo5 kuwa utekelezaji wa sheria hiyo si mgumu kama wengi wanavyodhani na infact wengi wataenda jela. “Ili sheria itekelezeke huhitaji kushtaki watu wote,” amesema Msando. “

“Huwezi ukakamatwa wewe umemtukana Albert ukasema na Abdalah alimtukana naye akamatwe. Ukikamatwa wewe tunaanza na wewe. Kwahiyo ukimuona mwenzio amefungwa miezi sita, miaka saba, miaka mitano, amelipishwa faini, definitely utaacha.”

“Kwasababu kazi ya sheria ni kwanza kumrekebisha mtu kwa njia ya adhabu na pili kumsababisha mtu aepuke kufanya jambo kitu fulani. Inapopitishwa ukiona watu wa kwanza wa pili kweli imetekelezeka, kuna watu wataacha zile tabia maake watajua sasa hapa ni tatizo. Na umeangalia kabla hata haijatumika watu wanakuambiwa ‘tutukane ya mwisho mwisho kabla ya hiyo sheria haijaanza kupitia. Tayari watu wameshajua ni makosa kufanya mbili tatu.”

Msando amewataka watumiaji wa mitandao ya kijamii kuheshimiana na kuitumia kwaajili ya maendeleo na kupata taarifa sahihi.

“Mimi nimeitumia vizuri, nimepata wateja zaidi ya watano wa kazi kubwa tu kwa kupitia mitandao ya kijamii.”
 

Imehaririwa na;- Unknown

Habari yako! Endelea kutembelea Tovuti ya TeknoTaarifa kwa Taarifa murwa za Teknolojia kutoka ndani na nje ya Tanzania, Tupo kwa ajili ya wapenzi wa Teknolojia.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post