Header ads

Header ads
» » UTAFITI: Asilimia 41 ya wanawake katika ndoa, hawana mahusiano mazuri na Mama wakwe zao


asilimia 41 ya wanawake walio katika ndoa, hawana mahusiano mazuri baina yao na wakwe zao wa kike (mama wakwe)

Je unafahamu kuwa asilimia 41 ya wanawake hawazungumzi na mama wakwe zao. Asilima 41 hawana mahusiano mazuri na mama za wabwana zao. Hawazungumzi nao.
Utafiti unaonyesha kati ya wanawake 10, mmoja wao ana ugomvi na mama mkwe wake.
Utafiti uliofanywa na shirika la OnePoll la Uingereza unaonyesha kuwa ugomvi mkubwa kati ya mama mkwe na wake za vijana wao ni kutokana na usemi maarufu ” sisi zama zetu tulikuwa tunafanya hivi au vile ” .
Wanawake hawataki kuambiwa zama zile au kukosolewa mara kwa mara.
Utafiti huo pia unaonyesha kuwa nusu ya wanawake, washawalalamikia mabwana zao kuhusu kina mama zao, wazazi wa bwana wa kike.
Asilimia 15 ya wanawake wamewahi kukosana , ndoa kuvunjika kutokana na ugomvi kati ya mkwe na mama mkwe. Ugomvi mkubwa zaidi kati ya mke na mama mkwe kuhusu malezi ya watoto, wajukuu.

Imehaririwa na;- poatel Africa

Habari yako! Endelea kutembelea Tovuti ya TeknoTaarifa kwa Taarifa murwa za Teknolojia kutoka ndani na nje ya Tanzania, Tupo kwa ajili ya wapenzi wa Teknolojia.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post