Mfanyabiashara
maarufu Afrika, ambaye ni Mwenyekiti na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Viwanda
vya Dangote Group of Industries, Alhaji Aliko Dabgote akinyoosha mkono
kuangalia eneo la ufukwe wa Bahari ya Hindi katika Kijiji cha Mgao, Kata
ya Maumbu, Tarafa ya Mayanga, Mtwara Vijijini, ambapo atajenga bandari
yake ya kisasa kwa ajili kusafirisha saruji itakayozalishwa kwenye
kiwanda chake kikubwa kinachojengwa katika Kijiji cha Msijute.
Alhaji
Dangote akiwa na viongozi wa Kijiji cha Mgao pamoja na wananchi
akikagua uwanja heka mbili na nusu aliyopewa kwa ajili ya kujenga makazi
yake katika kijiji hicho
Mwenyekiti
wa Kijiji cha Mgao, Shaa (kushoto) akimuonesha Dangote eneo la uwanja
aliopewa na wanakijiji kwa ajili ya ujenzi wa mkazi yake. Kijiji nacho
kitanufaika na Dangote ambaye atawajengea shule, hospitali pamoja na
miradi mingine ya maendeleo.
Msafara wa Alhaji Dangote ukielekea eneo patakapojengwa Bandari.
Alhaji Dangote akishuka kwenye ndege na kulakiwa na Mwakilishi Mkazi wake hapa nchini, Esther Baruti
Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Halima Dendegu akisalimiana na Alhaji Dangote
Mkuu
wa Mkoa wa Mtwara, Halima Dedengu akimtambulisha Alhaji Dangote kwa
wananchi alipowasili katika Kijiji cha Mgao, ambapo amepewa Dangote
eneo la ujenzi wa Bandari
Mwenyekiti wa Kijiji cha Mgao, Shaa akihojiwa na wananchi kuhusu manufaa watakayopata wanakijiji endapo Nadari hiyo ikijengwa
Alhaji Dangote akizungumza na wanahabari kuhusu ujenzi wa bandari hiyo
Msafara wa Dangote ukitumia magari kutembelea kiwanda cha saruji kinachojengwa
Alhaji Dangote akiaga