Vyombo mbalimbali vya habari Vimetoa taarifa mbalimbali kuhusu Matukio ya kutisha yaliyotokea Uko Afrika Kusini kuhusu mashambulizi ya kibaguzi. Kulingana na baadhi ya habari kuenea katika mitandao ya kijamii kama Whatsapp na Facebook baadhi ya wageni wamepewa muda uliopangwa kuondoka vitongoji vikubwa katika Afrika Kusini au kuondoka kabisa kwenda kwenye Nchi zao.
Katika maeneo kama Johannesburg polisi wamelazimika kutumia risasi za moto, mabomu ya machozi na risasi za mpira kuzuia ghasia za kibaguzi. Wakazi wa Johannesburg walipora bidhaa za wafanya biashara wa kigeni.. Hadi sasa mashambulizi ya kibaguzi Watu 6 wameripotiwa kufa katika vurugu hizo.
Hizi ndizo sababu zinazosemekana kuwa Chanzo cha Vurugu hizo:
1. Kazi
Wakazi wa Afrika kusini wanadai wageni wanachukua ajira zao. Kulingana na takwimu za serikali kiwango cha ukosefu wa ajira nchini Afrika Kusini ni 25%.
2. Kuenea kwa Ukimwi
Wanachi wa Afrika kusini wanaamini kuongezeka kwa wageni ndio chanzo cha kuenea kwa Ugonjwa wa Ukimwi. Pia wanaaminika kuwa waamiaji wanawachukulia Wake zao na kutembea na wanawake wa Makabila tofauti nchini humo.
3. Ushindani
Na wageni wameleta ushindani mkubwa hususani katika Biashara. Pia wanaamini waamiaji ndio chanzo cha Kukosekana kwa rasilimali ili kuendeleza maisha, chakula na shughuli za makundi ya mtu binafsi na kusababisha kuzuka kwa mashambulizi hayo
.4. Mali
Baadhi wanaona Waamiaji ndio wanamiliki Mali kuliko wazawa wa Nchi hiyo.
5. Uhalifu
Idadi kubwa ya waamiaji wanashutumiwa kuongeza viwango vya uhalifu nchini. Kwa mujibu wa Rais Jacob Zuma ingawa raia wa kigeni wamekamatwa kwa makosa mbalimbali ni kupotosha kuhitimisha kwamba wageni wote wanashiliki katika uhalifu nchini.
6. Biashara
Raia wa kigeni wanaaminika kuchukua zaidi fursa kubwa ya biashara kuliko wazawa wa Nchi hiyo .
7. Ubaguzi (Exception)
idadi ya Waafrika Kusini wanaona kuwa wao ni bora kwa Waafrika wengine katika nchi ambavyo si vizuri na kuanza kuwabagua waamiaji hususani wanaotoka nchi za Afrika.
8. Uraia wa kipekee
Baadhi ya Waafrika Kusini wanataka fomu ya utaifa kwamba hisihusishe raia wengine wote kutoka nchi za Afrika.
9. utitiri wa wageni
Afrika Kusini imekuwa na idadi kubwa ya wageni toka nchi Mbalimbali za Afrika. Hii inatokana na kuruhusiwa kwa raia wengi wa kigeni kufanya makazi katika nchi hiyo ususani wanaokimbia vurugu na mgawanyiko wa kisiasa katika nchi zao.
10. Viongozi Wabovu
Viongozi wa mitaa ndio chanzo cha Machafuko hii ni baada ya kupanga mashambulizi makusudi dhidi ya Wageni
CREDIT: Abdallah Magana